Al-Maaida 5:94
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَيَبْلُوَنَّكُمُ ٱللَّهُ بِشَىْءٍ مِّنَ ٱلصَّيْدِ تَنَالُهُۥٓ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ ٱللَّهُ مَن يَخَافُهُۥ بِٱلْغَيْبِ ۚ فَمَنِ ٱعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Enyi mlioamini! Hakika Mwenyezi Mungu atawajaribu kwa kitu kidogo katika mawindo inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Mwenyezi Mungu amjue mwenye kumhofu katika ghaibu. Kwa hivyo, mwenye kuvuka mipaka baada ya hayo, basi ana adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mwenyezi Mungu atakujaribuni kidogo kwa wanyama wa kuwinda inayo wafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Mwenyezi Mungu amjue nani anaye mkhofu kwa ghaibu. Basi atakaye ruka mipaka baada ya hayo atapata adhabu kali. [94]
[94] Enyi mlio amini! Hakika Mwenyezi Mungu anakufanyieni mtihani wakati wa Hija kwa kukuharimishieni baadhi ya wanyama na ndege ambao mnaweza kuwawinda kwa wepesi kwa mikono yenu na mikuki yenu. Makusudio ni kutaka wajuulikane ambao wanamt'ii Mwenyezi Mungu ijapo kuwa hawaonekani na watu. Na wanao pindukia mipaka aliyo iweka Mwenyezi Mungu baada ya kuibainisha watakuja pata adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi ambao mlimuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, Allah Mtukufu Atawapa mtihani wa baadhi ya 1 Rudia 2:3 kwa ufafanuzi wa al-ghyb. viwindwa vya barani, watakaokuja karibu na nyinyi kwa namna isiyo ya kawaida muweze kuwashika wadogo wao bila kutumia silaha na kuwashika wakubwa wao kwa kutumia silaha, ili Allah Mtukufu Awajue, ujuzi uliyofunuka wazi kwa viumbe, wale wanaomuogopa Mola wao kwa ghaibu kwa kuwa wana yakini kuwa ujuzi wa Allah Mtukufu kuhusu wao umekamilika, na kwa hivyo waache kuwinda wakiwa katika hali ya iḥrãm (ihramu: kuingia kwenye ibada ya Hija au Umra). Basi yoyote mwenye kuvuka mpaka wake, baada ya maelezo haya, akafanya ujasiri wa kuwinda, na hali yeye yuko kwenye ihramu, anastahili adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net