Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 93

Al-Maaida 5:93

المائدة

لَيْسَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوٓا۟ إِذَا مَا ٱتَّقَوا۟ وَّءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ ثُمَّ ٱتَّقَوا۟ وَّءَامَنُوا۟ ثُمَّ ٱتَّقَوا۟ وَّأَحْسَنُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Hakuna ubaya juu ya wale walioamini na wakatenda mema kwa vile walivyovila (zamani) maadamu wakimcha Mungu na wakiamini na wakitenda mema, kisha wakamcha Mungu, na wakaamini, kisha wakamcha Mungu na wakafanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao mazuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Si dhambi juu ya walio amini na wakatenda mema kwa walivyo vila (zamani) maadamu wakichamngu na wakiamini na wakitenda mema, kisha wakachamngu, na wakaamini, kisha wakachamngu na wakafanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao mazuri. [93]

[93] Walio mkubali Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda mema, hawana dhambi kwa vyakula vya halali na vizuri wanavyo kula, wala vya haramu walivyo wahi kula zamani kabla hawajajua kuwa ni haramu, ikiwa wanamkhofu Mwenyezi Mungu na wakajitenga navyo vyakula hivyo baada ya kujua kuwa vinakatazwa. Kisha ikawa wao wakaendelea kumkhofu Mwenyezi Mungu na kuzikubali sharia zake, na kisha wakadumu katika khofu yao ya kumwogopa Mwenyezi Mungu katika kila hali, na wakawa wanafanya a'mali zao kwa usafi wa niya, na kwa njia ya ukamilifu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu huwalipa wenye ikhlasi katika vitendo vyao kwa kadri ya ikhlasi yao na a'mali yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waumini waliokunywa pombe kabla haijaharamishwa hawana dhambi kwa kufanya hilo, iwapo wataiacha, wakajikinga na mambo yanayomkasirisha Allah Mtukufu na wakatanguliza matendo mema yanayoonyesha kuwa wao wanamuamini Yeye na wana hamu Allah Mtukufu, aliyetukuka, Awe radhi nao, kisha wakazidi kumcha Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, na kumuamini mpaka wakawa, kwa ile yakini yao, wanamuabudu kama kwamba wao wanamuona. Hakika Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anawapenda wale ambao wamefikia kiwango cha ihsani (iḥsãn) mpaka wakawa kuiamini kwao ghaibu (al-ghayb) ni kama vile wanavyoyaamini wanayoyaona.(1)

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net