Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 92

Al-Maaida 5:92

المائدة

وَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ وَٱحْذَرُوا۟ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ

Maana

Na mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka, basi hakika jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe kuliko wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi. [92]

[92] Na fuateni amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume wake kwa yale anayo kuleteeni kutoka kwa Mola wake Mlezi. Na yaepukeni mbali yatakayo kuleteeni adhabu mnapo kwenda kinyume. Mkitofuata anayo kuamrisheni Mwenyezi Mungu kuweni na yakini kuwa Yeye atakupeni adabu. Wala nyinyi hamna udhuru wowote baada ya kuwa Mtume amekwisha wabainishieni adabu ya kupewa wakhalifu. Na hakika haimpasi Mtume wetu ila kukujuvyeni hukumu zetu tu, na kukubainishieni kwa ukamilifu wa uwazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Fuateni amri, enyi Waislamu, ya kumtii Allah Mtukufu na kumtii Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, katika kila mnalolifanya na mnaloliacha. Na mcheni Allah Mtukufu katika hayo. Na mkikataa kufuata amri na mkayafanya mliyokatazwa, basi jueni kuwa jukumu la mjumbe wetu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ni ufikishaji ulio wazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net