Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
Sura ya 5

Al-Maaida

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 92

وَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ وَٱحْذَرُوا۟ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ 92

{92} Kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake ni kitu kimoja. Mwenye kumtii Mwenyezi Mungu, basi hakika amemtii Mtume. Na mwenye kumtii Mtume, basi hakika amemtii Mwenyezi Mungu. Na hilo linajumuisha kutekeleza yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake miongoni mwa vitendo na maneno yaliyo dhahiri na yaliyofichikana, ya wajibu na yanayopendekezwa; yanayohusiana na haki za Mwenyezi Mungu na haki za viumbe vyake, na kujiepusha na yale ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamekataza pia. Na jambo hili ndilo amri ya ujumla zaidi kuliko zote, kwani kama unavyoona, kila amri na makatazo, ya dhahiri na yaliyofichikana. Na kauli yake, "na tahadharini;" yaani, kutokana na kumuasi Mwenyezi Mungu na kumuasi Mtume wake. Kwa maana katika hayo kuna uovu na hasara iliyo wazi. "Na ikiwa mtageuka;" mkaacha mliyoamrishwa na yale mliyokatazwa, "basi hakika jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe kuliko wazi." Na tayari alikwisha yatekeleza hayo. Kwa hivyo mkiongoka, basi ni kwa ajili ya nafsi zenu; na mkifanya ubaya, basi ni juu yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye atakayewahisabu, naye Mtume alikwisha tekeleza yale yaliyo juu yake na yale aliyobebeshwa.