Al-Maaida 5:9
المائدةوَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ ۙ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ
Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema kwamba wana kufutiwa dhambi na malipo makubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu amewaahidi walio muamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfira na malipo makubwa. [9]
[9] Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake amewaahidi walio isadiki Dini yake na wakatenda mema kuwa atawasamehe dhambi zao, na atawalipa badala yake thawabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewapa ahadi, wale ambao wamemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakatenda mema, kwamba Atawasamehe madhambi yao na Atawalipa Pepo kwa hilo. Na Allah Mtukufu Haendi kinyume na ahadi Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net