Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 10

Al-Maaida 5:10

المائدة

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَحِيمِ

Maana

Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha Ishara zetu, hao ndio watu wa Jahiim.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio kufuru na wakakanusha Ishara zetu, hao ndio watu wa Motoni. [10]

[10] Na wale wanayo ipinga Dini ya Mwenyezi Mungu, na wakakanusha Ishara zinazo onyesha Umoja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ukweli wa Ujumbe wake, hao ni watu wa kudumu katika Jahannamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliokanusha upweke wa Allah Mtukufu unaoijulisha haki iliyo waziwazi na wakazikanusha dalili zake walizokuja nazo Mitume, hao ndio watu wa Motoni watakaosalia humo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net