Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 11

Al-Maaida 5:11

المائدة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَن يَبْسُطُوٓا۟ إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, walipotaka watu kuwanyooshea mikono yao, naye akaizuia mikono yao kuwafikia. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na kwa Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, walipo taka watu kukunyooshieni mikono, naye akaizuilia mikono yao kukufikieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. [11]

[11] Enyi Waumini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu katika wakati wa shida, pale baadhi ya Washirikina walipo kusudia kukuuweni nyinyi na Mtume wenu, Mwenyezi Mungu akazuia balaa yao isikufikieni, na akakuokoeni. Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na mumtegemee Yeye peke yake, katika mambo yenu. Kwani Yeye anakutosheni. Inavyo muelekea Muumini ni kumtegemea Mwenyezi Mungu peke yake daima milele.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mlimuamini Allah Mtukufu na Mtume wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, yakumbukeni yale Aliyowaneemesha Allah Mtukufu, miongoni mwa neema ya usalama, kutia uoga kwenye nyoyo za maadui zenu waliotaka kuwavamia, Allah Mtukufu Akawaepusha na nyinyi na Akaweka kizuizi kati yao na yale waliyoyataka kwenu. Na mcheni Allah Mtukufu, Na mtegemeeni Allah Mtukufu, Peke Yake, katika mambo yenu ya kidini na ya kidunia na muwe na hakika ya kupata msaada Wake na uokozi Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net