Al-Maaida 5:7
المائدةوَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَـٰقَهُ ٱلَّذِى وَاثَقَكُم بِهِۦٓ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, na agano lake alilofungamana nanyi, mliposema: Tumesikia na tumetii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua sana yaliyo ndani ya vifua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, na ahadi yake aliyo fungamana nanyi mlipo sema: Tumesikia na tumet'ii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa yaliyomo vifuani. [7]
[7] Kumbukeni, enyi Waumini, neema za Mwenyezi Mungu alizo kuneemesheni kwa kukuongoeni kwenye Uislamu. Jitahidini kutimiza ahadi yake aliyo itaka kwenu wakati mlipo muunga mkono Mtume wake, Muhammad, kuwa mtamsikia na mtamt'ii. Na mcheni Mwenyezi Mungu kwa kuzihifadhi ahadi hizi. Yeye, Subhanahu, ni Mjuzi sana wa yote yaliyo fichikana nyoyoni mwenu, naye atakulipeni kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni neema ya Allah Mtukufu kwenu katika sheria Yake Aliyowaekea na kumbukeni ahadi Yake Yeye Aliyetukuka, Aliyoichukua kwenu ya kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kuwasikiliza na kuwatii. Na mcheni Allah Mtukufu katika Aliyowaamrisha na Aliyowakataza. Hakika Allah Mtukufu ni Mjuzi wa mnayoyaficha katika nafsi zenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net