Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 63

Al-Maaida 5:63

المائدة

لَوْلَا يَنْهَىٰهُمُ ٱلرَّبَّـٰنِيُّونَ وَٱلْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ ٱلْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ ٱلسُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا۟ يَصْنَعُونَ

Maana

Mbona hao wanachuoni wa Kiyahudi na makuhani wao hawawakatazi kusema kwao dhambi, na kula kwao vya haramu? Ni maovu mno hayo wayafanyayo!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mbona hao wanazuoni na makohani wao hawawakatazi maneno yao ya dhambi, na ulaji wao vya haramu? Ni maovu mno hayo wayafanyayo! [63]

[63] Si ingelikuwa vyema lau kuwa wanazuoni wao na makohani wangeli wakataza kusema uwongo, na kula haramu? Uwovu mkubwa huo wanao ufanya kwa kuacha kusemezana na kukatazana maasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mbona viongozi wao na wasomi wao hawawakatazi hawa ambao wanayakimbilia madhambi na kufanya uadui, kusema urongo, uzushi na kula mali za watu kinyume na haki? Ni kiovu mno walichokifanya, walipoacha kukataza munkar (mabaya).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net