Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 62

Al-Maaida 5:62

المائدة

وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ وَأَكْلِهِمُ ٱلسُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Na utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia kwenye dhambi, na kupita mipaka, na ulaji wao vya haramu. Ni maovu mno hayo wayatendayo!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi, na uadui, na ulaji wao vya haramu. Ni maovu mno hayo wayatendayo! [62]

[62] Na utawaona wengi wao hawa wanakimbilia kufanya maasi na kuwatendea uadui wengineo, na pia katika kula mali ya haramu kama rushwa (mrungura) na riba! Uwovu gani huu wautendao!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na utawaona, ewe Mtume, wengi miongoni mwa Mayahudi wanayakimbilia maasia ya kusema urongo, uzushi, kuzifanyia uadui hukumu za Allah Mtukufu na kula mali ya watu kinyume na haki. Ni maovu mno matendo yao na uadui wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net