Al-Maaida 5:61
المائدةوَإِذَا جَآءُوكُمْ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا وَقَد دَّخَلُوا۟ بِٱلْكُفْرِ وَهُمْ قَدْ خَرَجُوا۟ بِهِۦ ۚ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا كَانُوا۟ يَكْتُمُونَ
Na wanapowajia, husema, "Tumeamini." na ilhali hakika waliingia na ukafiri wao, nao wameshatoka nao pia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema yale wanayoyaficha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo kujieni husema: Tumeamini. Lakini hakika wao wameingia na ukafiri wao, na wametoka nao pia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi kabisa wa yote wanayo yaficha. [61]
[61] Wanaafiki wakikujia husema uwongo, na hukwambia: Tumeamini. Nao wamekuingilia na hali ni makafiri, na wametoka kwenu nao ni makafiri vile vile! Na Mwenyezi Mungu anaujua vyema unaafiki wanao uficha. Na Yeye ndiye atakaye waadhibu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakiwajia nyinyi, enyi Waumini, wanafiki wa Kiyahudi husema, «Tumeamini,» na hali wao wako ukafirini na wanaendelea nao hakika wameingia kwenu wakiwa na ukafiri wanaouitakidi ndani ya nyoyo zao, kisha wametoka wakiwa bado wanaushikilia ukafiri huo. Allah Mtukufu ni Mjuzi zaidi wa siri zao hata wakionyesha kinyume cha hivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net