Al-Maaida 5:60
المائدةقُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ ٱلْقِرَدَةَ وَٱلْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّـٰغُوتَ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ
Sema: Je, niwaambie lililo baya zaidi kuliko hilo katika malipo mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu alimlaani na akamkasirikia, na akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shetani. Hao ndio wenye mahali pabaya zaidi na waliopotea zaidi njia iliyo sawa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Je! Nikwambieni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shet'ani. Hao ndio wenye mahali pabaya na wamepotea zaidi njia iliyo sawa. [60]
[60] Waambie: Nikwambieni malipo maovu kabisa kutokana na Mwenyezi Mungu? Ni hivyo vitendo vyenu nyinyi mlio tengwa mbali na Mwenyezi Mungu na rehema yake, na mkakasirikiwa kwa sababu ya ukafiri wenu na uasi wenu, na mkazibwa nyoyo zenu, mkawa kama manyani na nguruwe, na mkamuabudu Shetani, na mkafuata upotovu. Nyinyi ndio mko katika daraja ya mwisho katika shari, kwa sababu nyinyi ni watu walio potea kabisa, mkaiwacha Njia ya Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Nabii, kuwaambia Waumini, «Je, niwajulishe yule ambaye atalipwa, Siku ya Kiyama, malipo makali zaidi kuliko hawa wenye kutoka nje ya utiifu?» Hao ni waliowatangulia wao ambao Allah Mtukufu Aliwafukuza kwenye rehema Yake, Aliwakasirikia na akawageuza maumbile yao Akawafanya manyani na nguruwe kwa kuasi kwao, kuzua kwao urongo na kuwa na kiburi, kama ambavyo walikuwa kati yao wenye kuabudu Tãghût ( kila kinachoabudiwa badala ya Allah Mtukufu nacho kimeridhika). Hao, ni pabaya mno mahali pao huko Akhera; na harakati zao ulimwenguni zilikosa mwelekeo wa njia ya sawa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net