Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 59

Al-Maaida 5:59

المائدة

قُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّآ إِلَّآ أَنْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ أَكْثَرَكُمْ فَـٰسِقُونَ

Maana

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Je, mnatuchukia isipokuwa tu kwamba tulimuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa na yale yaliyoteremshwa kabla, na kwa kuwa wengi wenu ni wavukao mipaka?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hivyo mnatuchukia kwa kuwa tumemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo teremshiwa na yaliyo teremshwa kabla, na kwa kuwa wengi katika nyinyi ni wapotofu? [59]

[59] Sema ewe Mtume! Enyi Watu wa Kitbu! Hivyo mnatuchukia kwa kuwa tunamuamini Mwenyezi Mungu na tunaamini tuliyo teremshiwa sisi, nayo ni Qur'ani, na Vitabu vilio sahihi vilio teremshiwa Manabii wa zamani, na kwa kuwa tunaamini kuwa wengi wenu mmeitupa Sharia ya Mwenyezi Mungu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hao wanaofanya shere kati ya hao waliopewa Kitabu, «Mnalolikuta kuwa ni jambo la kutukanika au ni la aibu, hilo kwetu ni zuri kusifika nalo. Na hilo ni lile la kumuamini kwetu Allah Mtukufu na vitabu Vyake vilivyoteremshwa kwetu na waliokuwa kabla yetu na kuamini kwetu kwamba wengi wenu muko nje ya njia iliyonyooka».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net