Al-Maaida 5:58
المائدةوَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ ٱتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ
Na mnapoiadhinia Swala, wao wanaifanyia masihara na mchezo. Hayo ni kwa sababu wao ni kaumu wasiotumia akili.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mnapo adhinia Swala wao wanaichukulia maskhara na mchezo. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasio na akili. [58]
[58] Na katika kejeli zao kukufanyieni ni vile pale mnapo ita kwenda kuswali katika adhana, wao huifanyia maskhara Swala yenu, na hukuchekeni, wakafanya ni mchezo. Na hayo ni kwa sababu kuwa wao ni kaumu wasio na akili, wala hawatambui farka iliopo baina ya upotofu na uwongofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na anapoadhini mwadhini wenu, enyi Waumini, kuita watu kwenye Swala, Mayahudi, Wanaswara na washirikina wanafanya shere na kuukejeli mwito wenu wa hiyo Swala. Hii ni kwa sababu ya ujinga wao wa kutomjua Mola wao na kwa kuwa wao hawajui uhakika wa ibada.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net