Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 57

Al-Maaida 5:57

المائدة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلِكُمْ وَٱلْكُفَّارَ أَوْلِيَآءَ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Maana

Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wandani wale walioifanyia kejeli na mchezo Dini yenu miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu, na makafiri wengine. Na mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiwafanye marafiki wale walio ifanyia kejeli na mchezo Dini yenu miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, na makafiri wengine. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wenye kuamini. [57]

[57] Enyi mlio amini! Msiwafanye maadui wa Uislamu walio ifanyia maskhara Dini yenu wakaichezea - nao ni Mayahudi na Wakristo na washirikina, kuwa ndio wasaidizi, wala msifanye urafiki nao. Na mkhofuni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wakweli katika Imani yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mlimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, msiwafanye wale wanaoifanyia shere na kuichezea Dini yenu, miongoni mwa waliopewa Vitabu na makafiri, kuwa ni wasimamizi wa mambo yenu. Na muogopeni Allah Mtukufu mkiwa nyinyi mnamuamini Yeye na mnaziamini sheria Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net