Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 56

Al-Maaida 5:56

المائدة

وَمَن يَتَوَلَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فَإِنَّ حِزْبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ

Maana

Na mwenye kumfanya rafiki wandani Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndio wenye kushinda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na atakaye fanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda. [56]

[56] Na mwenye kufanya urafiki na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini na wakawa hao ndio wa kuwategemea kwa msaada na nusura, basi huyo atakuwa katika Hizbu (yaani kundi) ya Mwenyezi Mungu, na Hizbu ya Mwenyezi Mungu ndio yenye kushinda na kufuzu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mwenye kushikamana na Allah Mtukufu na akafuata muongozo wa Allah Mtukufu na Mtume Wake na akawa na muelekeo wa Waumini, basi yeye ni katika kundi la Allah Mtukufu, na kundi la Allah Mtukufu ndilo la washindi wenye kunusurika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net