Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 55

Al-Maaida 5:55

المائدة

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُمْ رَٰكِعُونَ

Maana

Hakika rafiki yenu mwandani ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka, nao wanarukuu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea. [55]

[55] Enyi Waumini! Urafiki wenu nyinyi uwe na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na nyinyi kwa nyinyi katika wanao shika Swala, na wanatoa Zaka, nao wananyenyekea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika msaidizi wenu, enyi Waumini, ni Allah Mtukufu na Mtume Wake na Waumini wanaojilazimisha na Swala za faradhi na wanatekeleza Zaka kwa hiari yao na hali wao ni wanyenyekevu kwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net