Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 54

Al-Maaida 5:54

المائدة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِۦ فَسَوْفَ يَأْتِى ٱللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُۥٓ أَذِلَّةٍ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ يُجَـٰهِدُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَآئِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Maana

Enyi mlioamini! Atakayeiacha Dini yake miongoni mwenu, basi Mwenyezi Mungu atakujaleta watu anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua. [54]

[54] Enyi mlio amini! Mwenye kurejea ukafirini katika nyinyi, baada ya kuamini, hamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Yeye ametukuka na hayo. Badala yao ataleta kaumu iliyo bora kuliko hao, na wao hao Mwenyezi Mungu atawapenda, na atawafikisha kwenye uwongofu, na ut'iifu. Na wao watampenda Mwenyezi Mungu, kwa hivyo watamt'ii. Nao watakuwa na unyenyekevu na huruma kwa ndugu zao Waumini, na watakuwa wakali na wenye nguvu mbele ya maadui zao makafiri. Watapigana jihadi kwa njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama yoyote ya mwenye kulaumu! Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye anaye muwafikia kheri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa fadhila kwa anaye stahiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata sheria zake kivitendo, Yoyote kati yenu atakayerudi nyuma akaiacha Dini yake, na akachukua badala yake dini ya Kiyahudi au ya Kinaswara au dini nyengineyo, basi hao hawatamdhuru Allah Mtukufu chochote; na Atawaleta watu bora kuliko wao: Anaowapenda na wanaompenda, wenye huruma kwa Waumini, wakali kwa makafiri, wanapigana jihadi na maadui wa Allah Mtukufu na hawamuogopi, kwa kumridhisha Allah Mtukufu, yoyote. Kuneemeshwa huko ni miongoni mwa nyongeza za Allah Mtukufu anazompa Amtakaye. Na Allah Mtukufu ni Mkunjufu wa fadhila, ni Mjuzi wa anayestahiki fadhila Zake katika waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net