Al-Maaida 5:51
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلْيَهُودَ وَٱلنَّصَـٰرَىٰٓ أَوْلِيَآءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُۥ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Enyi mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki wandani. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na mwenye kuwafanya marafiki wandani miongoni mwenu, basi huyo hakika ni miongoni mwao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. [51]
[51] Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwachukua Mayahudi na Wakristo mkawafanya ndio marafiki zenu. Wao hao ni sawa sawa katika kukufanyieni uadui. Na mwenye kufanya urafiki nao, basi ni kundi moja nao. Na hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi wanao jidhulumu nafsi zao kwa kufanya urafiki na makafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mlioamini, msiwafanye Mayahudi na Wanaswara ni washirika na wasaidizi wenu juu ya watu wa Imani. Hii ni kwa kuwa wao hawawapendi Waumini. Mayahudi wanasaidiana wao kwa wao, na hivyo hivyo ndivyo walivyo Wanaswara. Na makundi yote mawili yanakutana kwenye kuwafanyia nyinyi uadui. Na nyinyi, enyi Waumini, mnafaa zaidi kusaidiana nyinyi kwa nyinyi. Na yoyote mwenye kuwategemea wao katika nyinyi, basi yeye atakuwa ni miongoni mwao, na hukumu yake ni yao. Allah Mtukufu Hatawaafikia madhalimu wanaowategemea makafiri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net