Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 52

Al-Maaida 5:52

المائدة

فَتَرَى ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَـٰرِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰٓ أَن تُصِيبَنَا دَآئِرَةٌ ۚ فَعَسَى ٱللَّهُ أَن يَأْتِىَ بِٱلْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِۦ فَيُصْبِحُوا۟ عَلَىٰ مَآ أَسَرُّوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِمْ نَـٰدِمِينَ

Maana

Utawaona wale wenye maradhi katika nyoyo zao wanakimbilia kwao wakisema: 'Tunahofu kusibiwa na mabadiliko.' Basi huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo lingine kutoka kwake, na wakawa kwa yale waliyoyaficha katika nafsi zao ni wenye kujuta.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao. [52]

[52] Ilivyo kuwa kuwafanya hao marafiki hawafanyi ila walio dhulumu, basi utaona kuwa wanao wafanya makafiri ndio rafiki zao wana maradhi katika nyoyo zao, maradhi ya udhoofu na unaafiki. Wao husema: Tunaogopa usije kutupata msiba kwa kugeuka mambo na wao wasitusaidie! A'saa, huenda, Mwenyezi Mungu akamletea Mtume wake kufunguka mambo, na Waislamu wakawashinda maadui zao, au ukadhihiri unaafiki wa hao wanaafiki, wakaamkia majuto, wakijuta kwa zile kufuru na shaka shaka walizo kuwa wakizificha katika nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anasimulia habari ya kikundi cha wanafiki kwamba wao walikuwa wakikimbilia kupendana na Mayahudi kwa kuwa ndani ya nyoyo zao mulikuwa na shaka na unafiki, na walikuwa wakisema, «Sisi tunapendana nao kwa kuogopa wasije wakawashinda Waislamu wakatudhuru sisi pamoja na wao.» Allah Mtukufu, uliotukuka utajo Wake, Anasema: Huenda Allah Mtukufu Akauleta ushindi-yaani ushindi wa kuukomboa mji wa Makkah-, Akamnusuru Nabii Wake na Akaupa nguvu Uislamu na Waislamu juu ya makafiri au Akatayarisha mambo ambayo yataifanya iondoke nguvu ya Mayahudi na Wanaswara, na hapo waje wawanyenyekee Waislamu. Wakati huo watajuta wanafiki kwa yale waliyoyaficha kwenye nafsi zao ya kuwategemea Mayahudi na Wanaswara.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net