Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 50

Al-Maaida 5:50

المائدة

أَفَحُكْمَ ٱلْجَـٰهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ ٱللَّهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

Maana

Je, wanataka hukumu za Kijahiliya? Na ni nani aliye mzuri zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini? [50]

[50] Je, hao wanao kataa amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu wanataka wahukumiwe kwa hukumu ya Kijahiliya, ya kijinga, ya kabla ya kufika Uislamu, kulipo kuwa hapana uadilifu, bali matamanio ya nafsi tu ndiyo yliyo kuwa yakihukumu, na mapendeleo na udanganyifu ndio msingi wa hukumu? Huo ndio mwendo wa watu wa zama za Kijahiliya! Yuko aliye bora kuliko Mwenyezi Mungu kuhukumu watu wenye kuyakinika na Sharia na wenye kunyenyekea Haki? Kwa hakika hao ndio wanao tambua ubora wa hukumu za Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, wanataka Mayahudi hawa uhukumu kati yao kwa yale ya upotevu na ujinga waliyoyazoea washirikina wanaoabudu masanamu? Hayo hayawi wala hayafai kabisa. Na ni nani aliye muadilifu zaidi kuliko Allah Mtukufu katika hukumu Yake kwa aliyezifahamu sheria za Allah Mtukufu, akamuamini na akawa na yakini kwamba hukumu ya Allah Mtukufu ndiyo ya haki?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net