Al-Maaida 5:49
المائدةوَأَنِ ٱحْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَهُمْ وَٱحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَنۢ بَعْضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَٱعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَـٰسِقُونَ
Na hukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Na watahadhari wasije wakakutia majaribu ukaacha baadhi ya yale aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi miongoni mwa watu ni wenye kupita mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu. [49]
[49] Na wewe ewe Mtume! Tumekuamrisha uhukumu baina ya watu kwa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matakwa yao katika kuhukumu. Na wahadharishe wasije kukugeuza ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Pindi wakiipuuza hukumu ya Mwenyezi Mungu na wakataka nyengineyo, basi jua kuwa Mwenyezi Mungu anataka kuwapatiliza kwa kuwafisidia mambo yao, kwa vile zilivyo kwisha fisidika nafsi zao kwa sababu ya madhambi yao waliyo yatenda kwa kukhalifu hukumu zake na Sharia yake. Kisha atawalipa vitendo vyao vyote huko Akhera. Na hakika watu wengi ni wenye kuziasi hukumu za Sharia. Maneno haya yanatukuza Sharia ya Kiislamu katika kuwahukumu watu. Kwanza inatukuka kwa kuwa ni hukumu ya uadilifu na haifuati mipango ya watu ijapo kuwa ni mipotovu, bali inahukumu juu ya hiyo mipango ya watu kwa kheri na shari. Pili Kanuni huwa katika dola ni moja tu kwa watu wote na mat'abaka yote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hukumu, ewe Mtume, kati ya Mayahudi kwa Aliyokuteremshia Allah Mtukufu katika Qur’ani, wala usiyafuate matakwa ya wale wanaoshitakiana kwako. Na jihadhari nao wasikuzuie na baadhi ya Aliyokuteremshia Allah Mtukufu ukaacha kuyatumia. Na iwapo wataikataa hukumu unayoitoa, basi jua kwamba Allah Mtukufu Anataka kuwaepusha na njia ya uongofu kwa sababu ya madhambi waliyotangulia kuyafanya. Na kwa hakika, wengi wa watu wako nje ya utiifu wa Mola wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net