Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 47

Al-Maaida 5:47

المائدة

وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ ٱلْإِنجِيلِ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ

Maana

Basi na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na mwenye kutohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio waliopita mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu. [47]

[47] Na Sisi tuliwaamrisha wafuasi wa Isa, yaani Watu wa Injili, Wakristo, wahukumu kwa hukumu alizo teremsha Mwenyezi Mungu. Na wasio hukumu kwa mujibu wa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu basi hao wameiacha Sharia ya Mwenyezi Mungu, ni waasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi na wahukumu watu wa Injili, ambao alitumwa kwao ‘Ǐsâ, kwa yaliyoteremshwa na Allah Mtukufu ndani yake. Na wale ambao hawakuhukumu kwa yaliyoteremshwa na Allah Mtukufu, Basi hao ndio wenye kutoka kwenye amri Yake, wenye kumuasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net