Al-Maaida 5:46
المائدةوَقَفَّيْنَا عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِم بِعِيسَى ٱبْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ ۖ وَءَاتَيْنَـٰهُ ٱلْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ
Na tukawafuatishia nyuma yao, Isa mwana wa Maryam akiyasadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyo na uongofu ndani yake, na ni nuru, na inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na ni uwongofu na mawaidha kwa wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu. [46]
[46] Na baada ya hawa Manabii tulimtuma Isa mwana wa Maryamu, naye ni mwenye kufuata njia yao, na kuithibitisha Taurati iliyo mtangulia. Naye tulimteremshia Injili yenye uwongofu kuelekea Haki, na yenye kubainisha hukumu, na tuliiteremsha ili isadikishe Taurati iliyo tangulia, na ndani yake pana uwongofu wa kupelekea Haki, na ni mawaidha kwa wachamngu. (Tazama Injili ya Mathayo 5.17 maneno ya Nabii Isa: "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.")
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukawafuatishia, Manabii wa Wana wa Isrãîl, ‘Ǐsâ mwana wa Maryam akiwa ni mwenye kuyaamini yaliyomo ndani ya Taurati na kuzitumia hukumu zilizomo kati ya zile ambazo hazikufutwa na Kitabu chake na tukamteremshia Injili ikiwa ni yenye kuongoza kwenye haki na yenye kuyaeleza yale ambayo watu hawakuyajua katika hukumu za Allah Mtukufu na ni yenye kutoa ushahidi juu ya ukweli wa Taurati kwa hukumu zake ilizokusanya Na tumeifanya ni bainifu kwa wale wanaomuogopa Mola wao, ni yenye kuwakemea wasiyafanye yaliyoharamishwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net