Al-Maaida 5:45
المائدةوَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَآ أَنَّ ٱلنَّفْسَ بِٱلنَّفْسِ وَٱلْعَيْنَ بِٱلْعَيْنِ وَٱلْأَنفَ بِٱلْأَنفِ وَٱلْأُذُنَ بِٱلْأُذُنِ وَٱلسِّنَّ بِٱلسِّنِّ وَٱلْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُۥ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Na humo tuliwaandikia ya kwamba nafsi kwa nafsi, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na kwa majeraha ni kisasi. Lakini mwenye kuitoa kama sadaka, basi hiyo ni kafara kwake. Na yule asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na humo tuliwaandikia ya kwamba roho kwa roho, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na kwa majaraha kisasi. Lakini atakaye samehe basi itakuwa ni kafara kwake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu. [45]
[45] Tumewalizimisha Mayahudi katika Taurati wafuate sharia ya kisasi kwa ajili ya kuhifadhi maisha ya watu. Basi tukahukumu mwenye kuuwa auwawe. Mwenye kutofoa jicho la mtu atofolewe. Kadhaalika pua kwa pua, sikio kwa sikio, jino kwa jino, na jaraha hivyo hivyo lilipiziwe kisasi ikimkinika. (Hiyo ni hukumu ya Mayahudi kama ilivyo katika Kutoka 21.23-25; Mambo ya Walawi 24.18-21; Kumbukumbu la Torati 19.21. Katika Uislamu ipo fursa ya msamaha.) Mwenye kusamehe akatolea sadaka ile haki ya kulipiza kisasi kwa mkhalifu, basi hiyo sadaka huwa ni kafara kwake. Mwenyezi Mungu naye atamfutia sehemu ya madhambi yake. Na watu wasio hukumu kwa mujibu wa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulilifanya ni lazima kwao katika Taurati kwamba mtu huuawa akiua mtu, hutolewa jicho akitoa jicho la mtu, hukatwa pua akikata pua ya mtu, hukatwa sikio akikata sikio la mtu, na hung’olewa jino aking’oa jino la mtu na kwamba hulipizwa kisasi kwa kutia mtu majaraha. Mwenye kusamehe haki yake ya kulipiza kisasi kwa aliyemfanyia uadui, basi huko ni kujifutia na kujiondolea sehemu ya madhambi ya yule aliyefanyiwa uadui. Na yule asiyehukumu kwa yaliyoteremshwa na Allah Mtukufu, katika kisasi na megineyo, basi hao ni wakiukaji wa mipaka ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net