Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 31

Al-Maaida 5:31

المائدة

فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِى ٱلْأَرْضِ لِيُرِيَهُۥ كَيْفَ يُوَٰرِى سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَـٰوَيْلَتَىٰٓ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا ٱلْغُرَابِ فَأُوَٰرِىَ سَوْءَةَ أَخِى ۖ فَأَصْبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ

Maana

Hapo Mwenyezi Mungu akamtuma kunguru anayefukua katika ardhi ili amwonyeshe jinsi ya kuuzika mwili wa kaka yake. Akasema: 'Ole wangu! Nimeshindwa kuwa kama kunguru huyu nikauzika mwili wa kaka yangu?' Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anaye fukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi kumsitiri nduguye. Akasema: Ole wangu! Nimeshindwa kuwa kama kunguru huyu nikamsitiri ndugu yangu? Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta. [31]

[31] Baada ya kumuuwa yakamjia majuto na kubabaika. Akawa hajui amfanyeje maiti! Mwenyezi Mungu akampeleka kunguru akafukua udongo amzike kunguru mwengine aliye kufa, ili amfunze muuwaji vipi kumsitiri mwenzake aliye kwisha kufa. Alipo hisi uovu wa aliyo yatenda, alijuta kwa ukhalifu wake, akasema: Nimeshindwa hata kuwa kama kunguru huyu nikamsitiri ndugu yangu? Akawa basi miongoni wa walio juta kwa makosa yake, na kwenda kinyume na yanavyo takikana na maumbile.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Qãbîl alipomuua ndugu yake, hakujua aufanye nini mwili wake. Hapo Allah Mtukufu Alimtuma kunguru, akawa anafukua shimo katika ardhi ili amzike humo kunguru aliyekufa, ili amjulishe Qãbîl namna ya kuuzika mwili wa ndugu yake. Qãbîl alistaajabu na akasema, «Kwani nimeshindwa kufanya vile kunguru huyu alivyofanya nikapata kuificha aibu ya ndugu yangu?» Hapo Qãbîl alimzika ndugu yake. Na baada ya hasara aliyorudi nayo, Allah Mtukufu alimpa mateso ya majuto.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net