Al-Maaida 5:30
المائدةفَطَوَّعَتْ لَهُۥ نَفْسُهُۥ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُۥ فَأَصْبَحَ مِنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ
Basi nafsi yake ikampelekea kumuua kaka yake, na akamuua. Kwa hivyo akawa miongoni mwa waliohasirika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika. [30]
[30] Basi nafsi yake ilimsahilishia kukhalifiana na maumbile, kumuuwa nduguye, akamuuwa. Kwa hivyo akawa kwa mujibu wa hukumu ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa walio khasiri, kwa kuwa ameipoteza imani yake na amempoteza nduguye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi ilimpambia Qãbîl nafsi yake amuue ndugu yake, akamuua na akawa ni kati ya waliopata hasara, ambao waliuza Akhera yao kwa dunia yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net