Al-Maaida 5:29
المائدةإِنِّىٓ أُرِيدُ أَن تَبُوٓأَ بِإِثْمِى وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلنَّارِ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَٰٓؤُا۟ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Hakika mimi ninataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako, ili wewe uwe miongoni mwa watu wa Motoni. Na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako, kwani wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Na hayo ndiyo malipo ya wenye kudhulumu. [29]
[29] Mimi sitakuzuia utapo taka kuniuwa ili upate kubeba dhambi za kuniuwa mimi pamoja na dhambi zako za tangu hapo za kutomsafia niya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wewe unastahiki huko Akhera kuwa katika watu wa Motoni. Na hayo ni malipo ya haki ya Mwenyezi Mungu kumlipa kila mwenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Mimi nataka urudi ukiwa umebeba dhambi la kuniua mimi na dhambi lililokuwa juu yako kabala ya hilo, upate kuwa ni miongoni mwa watu wa Motoni na watakaosalia humo. Na hayo ndiyo malipo ya wanaofanya uadui».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net