Al-Maaida 5:28
المائدةلَئِنۢ بَسَطتَ إِلَىَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِى مَآ أَنَا۠ بِبَاسِطٍ يَدِىَ إِلَيْكَ لِأَقْتُلَكَ ۖ إِنِّىٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Ukininyooshea mkono wako ili uniue, mimi sitakunyooshea mkono wangu ili nikuue. Hakika mimi namhofu Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ukininyooshea mkono wako kuniuwa, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote. [28]
[28] Akamwambia: Shetani akikuzuga hata ukaninyooshea mkono ili kuniuwa, mimi sitofanya kama hivyo, wala sitanyoosha mkono wangu kwa ajili ya kukuuwa. Hakika mimi naogopa adhabu ya Mola wangu Mlezi, naye ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hãbîl akasema, akimpa mawaidha ndugu yake, «Iwapo utaunyosha mkono wako kwangu ili uniue, hutapata kutoka kwangu mfano wa kitendo chako. Mimi namuogopa Allah Mtukufu mola wa viumbe wote».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net