Al-Maaida 5:27
المائدةوَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ٱبْنَىْ ءَادَمَ بِٱلْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ ٱلْـَٔاخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلْمُتَّقِينَ
Na wasomee habari za wana wawili wa Adam kwa haki. Walipotoa mhanga, basi ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwingine haukukubaliwa. Akasema (yule ambaye haukukubaliwa mhanga wake): Lazima nitakuua. Akasema huyo mwingine: Hakika Mwenyezi Mungu hupokea tu kutoka kwa wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu. [27]
[27] Hakika kupenda kutenda uadui ni tabia ya baadhi ya watu. Basi ewe Nabii! Wasomee Mayahudi - na wewe ni msema kweli - khabari za Haabila na Qaabila, wana wawili wa Adam. Kila mmoja alichinja dhabihu kama ni mhanga kwa kutaka kuruba kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu alimkubalia mmoja kwa ajili ya usafi wa niya yake, na akamkatalia wa pili kwa kuwa niya yake haikuwa safi. Basi yule aliye kataliwa akamhusudu mwenzie na akamuahidi kuwa atamuuwa. Yule nduguye akamrudi kwa kumbainishia kuwa Mwenyezi Mungu hapokei a'mali ila kwa wachamngu walio safisha niya zao katika kule kutafuta kuruba.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wasimulie, ewe Mtume, Wana wa Isrãîl habari ya wana wawili wa Ãdam, Qãbîl na Hãbîl, nayo ni habari ya kweli, alipotoa kila mmoja wao sadaka, nayo ni ile inayotolewa ili kujisogeza karibu kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Hapo Allah Mtukufu Aliikubali sadaka ya Hãbîl kwa kuwa alikuwa mcha-Mungu, na Hakuikubali sadaka ya Qãbîl, kwa kuwa hakuwa mcha-Mungu.Qãbîl alimhusudu ndugu yake na akasema, «Nitakuua.» Hãbîl akajibu, «Kwa hakika Allah Mtukufu Huikubali sadaka itokayo kwa wale wenye kumuogopa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net