Al-Maaida 5:26
المائدةقَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ ۛ أَرْبَعِينَ سَنَةً ۛ يَتِيهُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ فَلَا تَأْسَ عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْفَـٰسِقِينَ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi hakika nchi hiyo wameharamishiwa, kwa muda wa miaka arobaini watakuwa wakitangatanga katika ardhi. Basi wewe usiwasikitikie watu wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi nchi hiyo wameharimishiwa muda wa miaka arubaini, watakuwa wakitanga-tanga katika ardhi. Basi wewe usiwasikitikie watu wapotovu. [26]
[26] Mwenyezi Mungu akamuitikia Musa, akawapigia marfuku hao wakhalifu wasiingie nchi hiyo kwa muda wa miaka arubaini, wakipotea ovyo majangwani hawajui wendako wala watokako. Mwenyezi Mungu akamwambia Musa kama kumuasa: Usisikitike kwa masaibu yaliyo wasibu, kwani hawa ni wapotovu, wameiasi amri ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Alisema kumwambia Nabii Wake Mûsã, amani imshukie, «Hakika hiyo ardhi takatifu ni haramu kwa hawa Mayahudi kuiingia kwa muda wa miaka arubaini, watakuwa wakitanga katika ardhi wakiwa kwenye hali ya mshangao. Basi usiwasikitikie, ewe Mûsã, watu waliotoka kwenye utiifu wangu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net