Al-Maaida 5:25
المائدةقَالَ رَبِّ إِنِّى لَآ أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِى وَأَخِى ۖ فَٱفْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ ٱلْقَوْمِ ٱلْفَـٰسِقِينَ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi similiki isipokuwa nafsi yangu na kaka yangu. Basi tutenge na hawa watu wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu. Basi tutenge na hawa watu wapotovu. [25]
[25] Hapo tena Musa akamrejea Mola wake Mlezi akisema: Mola wangu Mlezi! Sina madaraka ila juu ya nafsi yangu na ndugu yangu. Basi tuhukumie baina yetu na hawa watu wakaidi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mûsã alielekea kwa Mola wake akiomba, «Mimi sina uwezo isipokuwa wa nafsi yangu na ndugu yangu, basi hukumu kati yetu na watu wenye kuasi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net