Al-Maaida 5:24
المائدةقَالُوا۟ يَـٰمُوسَىٰٓ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَآ أَبَدًا مَّا دَامُوا۟ فِيهَا ۖ فَٱذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَـٰتِلَآ إِنَّا هَـٰهُنَا قَـٰعِدُونَ
Wakasema: Ewe Musa! Hakika Sisi kamwe hatutaingia humo maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane. Sisi hakika tutakaa papa hapa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Ewe Musa! Sisi hatutaingia humo kamwe maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane. Sisi tutakaa hapa hapa. [24]
[24] Lakini wakakakamia katika ukhalifu wao. Wakasema: Ewe Musa! Sisi bila ya shaka yoyote tumekwisha azimia kuwa hatutaingia nchi hii kabisa, maadamu wamo hao majabari. Basi tuache na yetu; kwani wewe huna madaraka yoyote juu yetu. Nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane nao hao majabari. Sisi tutakaa hapa hapa hatubanduki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu wa Mûsã walisema kumwambia, «Hatutaungia mji huo kabisa, iwapo hao majabari wamo humo. Hivyo basi, nenda wewe na Mola wako mkapigane. Ama sisi, tunakaa hapa- hapa na hatutapigana na wao.» Hii inaonesha kushikilia kwao kuenda kinyume na Mûsã, amani imshukie.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net