Al-Maaida 5:23
المائدةقَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمَا ٱدْخُلُوا۟ عَلَيْهِمُ ٱلْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَـٰلِبُونَ ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓا۟ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Wanaume wawili miongoni mwa wale wanaohofu ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, wakasema: Waingilieni mlangoni. Na mtakapowaingilia, basi kwa yakini nyinyi mtashinda. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watu wawili miongoni mwa wachamngu ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, walisema: Waingilieni kwa mlangoni. Mtakapo waingilia basi kwa yakini nyinyi mtashinda. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini. [23]
[23] Wawili kati ya wakubwa wao walio kuwa wanamwogopa Mwenyezi Mungu, na ambao Mwenyezi Mungu amewapa neema ya imani na ut'iifu, walisema: Enyi watu! Waingilieni hao majabari wa mjini kwa kupitia mlangoni kwa ghafla. Mkifanya hivyo nyinyi mtawashinda. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu peke yake katika mambo yenu yote, ikiwa nyiny ni wenye Imani ya kweli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walisema watu wawili kati ya wale wanaomuogopa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ambao Allah Mtukufu Aliwapa neema kwa kumtii kwao Yeye na kumtii Mtume Wake, kuwaambia Wana wa Isrãîl, «Ingieni kwa majabari hao kupitia lango la mji wao, ikiwa ni mojawapo ya njia za kutafuta sababu za ushindi. Mtakapoingia langoni, mtawashinda. Na kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, jitegemezeni, iwapo nyinyi mnamuamini Mtume Wake katika yale Aliyowaletea, mnaifuata sheria Yake kivitendo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net