Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 120

Al-Maaida 5:120

المائدة

لِلَّهِ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌۢ

Maana

Ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo ndani yake. Naye ni Muweza mno wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Naye ni Muweza wa kila kitu. [120]

[120] Ufalme wa mbinguni na katika ardhi na vyote viliomo humo ni wa Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye peke yake ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa, na Yeye tu ndiye Mwenye uweza ulio timia kutekeleza kila alitakalo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni wa Allah Mtukufu Peke Yake ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo ndani yake, na Yeye, Aliyetakata na kila sifa mbaya, kwa kila kitu ni muweza; hakuna kitu kinachomshinda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net