Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 119

Al-Maaida 5:119

المائدة

قَالَ ٱللَّهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ ٱلصَّـٰدِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۚ رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Maana

Mwenyezi Mungu akasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao ukweli utawafaa ukweli wao. Wao wana Mabustani yapitayo mito chini yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao walimridhia. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa. [119]

[119] Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Watapata mabustani yanayo pitiwa na mito chini ya miti yake. Na humo watakaa, wala hawatatoka milele, wakistarehe humo kwa radhi ya Mwenyezi Mungu anavyo waridhia wao, na wao watavyo kuwa radhi kwa malipo alio walipa. Na Neema hiyo ndio kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Atamwambia ‘Ǐsâ Siku ya Kiyama, «Hii ndiyo Siku ya Malipo ambayo kutawafaa wale waliompwekesha Allah Mtukufu kule kumpwekesha kwao Mola wao na kufuata kwao sheria Yake, ukweli wao wa nia zao, maneno yao na matendo yao. Watakuwa na mabustani ya Pepo, inayopita mito chini ya majumba yake ya fahari, hali ya kukaa humo milele. Allah Mtukufu Ameridhika nao ndipo Akayakubali mema yao, na wao wameridhika na Yeye kwa malipo mazuri mengi aliyowapa. Malipo hayo na kuwa Yeye Ameridhika na wao ndiko kufuzu kukubwa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net