Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 115

Al-Maaida 5:115

المائدة

قَالَ ٱللَّهُ إِنِّى مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّىٓ أُعَذِّبُهُۥ عَذَابًا لَّآ أُعَذِّبُهُۥٓ أَحَدًا مِّنَ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Mwenyezi Mungu akasema: Hakika Mimi nitawateremshia hicho. Lakini yeyote katika nyinyi atakayekufuru baadaye, basi hakika Mimi nitamuadhibu adhabu nisiyomuadhibu yeyote katika walimwengu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu akasema: Hakika Mimi nitakuteremshieni hicho. Lakini yeyote katika nyinyi atakaye kanya baadae, basi hakika Mimi nitampa adhabu nisiyopata kumpa yeyote katika walimwengu. [115]

[115] Mwenyezi Mungu akamwambia: Mimi nitakuteremshieni chakula kutoka mbinguni. Lakini mtu yeyote atakaye pinga neema hii baada ya kuteremka, basi Mimi nitampa adabu ambayo sijapata kumpa mtu yeyote. Kwani huyo atakuwa anakanya baada ya kwisha shuhudia dalili ya Imani aliyo itaka mwenyewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, aliyetukuka, Akasema, «Mimi ni Mwenye kuwateremshia Meza ya chakula. Basi yoyote mwenye kuukanusha upweke wangu, miongoni mwenu, na unabii wa ‘Ǐsâ, amani imshukie, baada ya kuteremka meza, nitamuadhibu adhabu kali ambayo sitamuadhibu nayo yoyote miongoni mwa viumbe.» Meza iliteremka kama alivyoahidi Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net