Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 114

Al-Maaida 5:114

المائدة

قَالَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ ٱللَّهُمَّ رَبَّنَآ أَنزِلْ عَلَيْنَا مَآئِدَةً مِّنَ ٱلسَّمَآءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَءَاخِرِنَا وَءَايَةً مِّنكَ ۖ وَٱرْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Maana

Akasema Isa mwana wa Maryam: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshie meza yenye chakula kutoka mbinguni ili kiwe kwetu Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora zaidi wa wanaoruzuku.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku. [114]

[114] Isa akawaitikia, na akasema: Ewe Mola wetu Mlezi, uliye miliki mambo yetu yote! Tuteremshie chakula kutoka mbinguni, kiwe ni siku-kuu kwetu kitapo teremka kwa walio amini miongoni mwetu, kwa walio tangulia na walio taakhari, na kiwe ni muujiza wa kutilia nguvu wito wako, na uturuzuku riziki njema, na Wewe ndiye Mbora wa kuruzuku.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

‘Ǐsâ mwana wa Maryam Aliyakubali matakwa ya Ḥawãriyyûn akamuomba Mola wake, Aliyetukuka na kuwa juu, kwa kusema, «Mola wetu! Tuteremshie meza ya chakula kutoka mbinguni, tupate kuifanya siku hiyo ya kuteremka kwake ni sikukuu kwetu, sisi tutaitukuza na pia watakaokuja baada yetu, na hiyo meza itakuwa ni alama na ni hoja kutoka kwako, ewe Allah Mtukufu, juu ya upweke wako na juu ya ukweli wa unabii wangu, na ututunuku miongoni mwa vipewa vyako vyingi, na wewe ndiye bora wa wenye kuruzuku».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net