Al-Maaida 5:113
المائدةقَالُوا۟ نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
Wakasema: Tunataka kula kwayo, na nyoyo zetu zitue, na tujue kwamba umetuambia ukweli, na tuwe miongoni mwa wanaoshuhudia juu ya hilo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Tunataka kukila chakula hicho, na nyoyo zetu zitue, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe miongoni mwa wanao shuhudia. [113]
[113] Wakasema: Hakika sisi tunataka kula katika chakula hicho, ili nyoyo zetu zitue kwa kudra ya Mwenyezi Mungu tunayo iamini, na tujue kwa kuona kwa macho ya kuwa hakika ni kweli hayo unayo twambia yanatoka kwake Subhanahu, Aliye takasika, na tupate kutoa ushahidi kwa muujiza huu kwa hao ambao hawakuuona.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ḥawãriyyûn wakasema, «Tunataka kula kutoka kwenye meza hiyo, nyoyo zetu zipate kutulia kwa kuishuhudia, tupate kujua kwa yakini ukweli wako kuhusu unabii wako na tupate kuwa ni wenye kuishuhudia miujiza hii kwamba Allah Mtukufu Ameiteremsha iwe ni hoja kwetu juu ya upweke Wake na uwezo Wake kufanya Alitakalo na pia iwe ni hoja kwako juu ya ukweli kuhusu unabii wako».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net