Al-Maaida 5:112
المائدةإِذْ قَالَ ٱلْحَوَارِيُّونَ يَـٰعِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَآئِدَةً مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ۖ قَالَ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Wanafunzi (wako) waliposema: Ewe Isa mwana wa Maryam! Je, Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia meza yenye chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanafunzi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini. [112]
[112] Ewe Nabii! Taja pia yaliyo tokea pale wafuasi wa Isa wenye ikhlasi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Hivyo Mola wako Mlezi atakuitikia ukimtaka akuteremshie chakula kutoka mbinguni? Isa akawaambia kuwajibu: Kama nyinyi ni kweli mnamuamini Mwenyezi Mungu, basi mkhofuni Yeye, na fuateni amri zake na makatazo yake. Wala msitafute hoja ila nilizo kuleteeni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ukumbuke waliposema Ḥawãriyyûn (wafuasi wa Nabii ‘Ǐsâ kati ya wafuasi wake), «Ewe ‘Ǐsâ mwana wa Maryam! Je, Anaweza Mola wako, kututeremshia meza ya chakula kutoka mbinguni?» akasema (Nabii Isa) muogopeni Allah Mtukufu kwa kujikinga na adhabu zake ikiwa ni wenye kuamini Imani ya kikweli.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net