Al-Maaida 5:111
المائدةوَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى ٱلْحَوَارِيِّـۧنَ أَنْ ءَامِنُوا۟ بِى وَبِرَسُولِى قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا وَٱشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ
Na nilipowafunulia ufunuo (wahyi) Wanafunzi (wako) kwamba: "Niaminini Mimi na Mtume wangu." Wakasema: "Tumeamini, na shuhudia kuwa sisi hakika ni Waislamu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nilipo wafunulia Wanafunzi kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu. [111]
[111] Ewe Mtume! Watajie umma wako yaliyo tokea tulipo watia hima kikundi cha alio wataka Isa wamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake Isa, na wakamuitikia wakawa ndio Wanafunzi wake makhsusi, na wakasema: Tumeamini. Na shuhudia ewe Mola wetu Mlezi, kuwa sisi tumesafi niya zetu, na tunafuata amri zako, yaani Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ukumbuke, ewe ‘Ǐsâ, Nilipowapa ilhamu kwenye nyoyo za wafuasi (wako) Kuwa waniamini mimi na mtune wangu(isa) wakasema, «Tumeamini, ewe Mola wetu. Na ushuhudie kuwa sisi ni wenye kukunyenyekea na ni wenye kufuata kwa utiifu amri Yako».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net