Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 116

Al-Maaida 5:116

المائدة

وَإِذْ قَالَ ٱللَّهُ يَـٰعِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ ءَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ ٱتَّخِذُونِى وَأُمِّىَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ ٱللَّهِ ۖ قَالَ سُبْحَـٰنَكَ مَا يَكُونُ لِىٓ أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِى بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُۥ فَقَدْ عَلِمْتَهُۥ ۚ تَعْلَمُ مَا فِى نَفْسِى وَلَآ أَعْلَمُ مَا فِى نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّـٰمُ ٱلْغُيُوبِ

Maana

Na pale Mwenyezi Mungu aliposema: Ewe Isa mwana wa Maryamu! Je, wewe ndiye uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu wawili badala ya Mwenyezi Mungu? (Isa) akasema: Subhanaka (Wewe umetakasika)! Hainifailii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema, basi bila ya shaka umekwishayajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mwenye kujua vyema yale yaliyofichikana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana. [116]

[116] Ewe Nabii! Taja yatakayo tokea Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu atapo mwambia Isa bin Maryamu kauli ya kutangaza haki: Ati wewe ndiye uliye waambia: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu, na muache kumuabudu Mwenyezi Mungu wa pekee? Isa atasema: Mimi ninakutakasa mtakaso wa ukamilifu ya kuwa Wewe huna mshirika. Wala hainifalii mimi nitake jambo ambalo sina haki nalo hata chembe. Lau kuwa nimesema hayo, basi Wewe ungeli jua. Kwani Wewe unayajua yaliyo fichikana ndani ya nafsi yangu, licha yanayo dhihiri kwa kuyasema. Wala mimi siyajui unayo nificha. Hakika Wewe ndiye Mwenye ujuzi ulio enea kila kilicho fichikana na kilicho ghibu. (Wakristo wote wanamuabudu Yesu, na Wakatoliki wanamwomba Maryamu pia, na wanamwita: "Mama wa Mungu")

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka pindi atakaposema Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, «Ewe ‘Ǐsâ mwana wa Maryam! Kwani wewe uliwaambia watu, ‘nifanyeni mimi na mamangu kuwa ni waabudiwa badala ya Allah Mtukufu’?» ‘Ǐsâ akajibu, kwa kumtakasa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na kumuepusha na sifa za upungufu, «Haipasii kwangu kuwaambia watu yasiyokuwa haki. Nikiwa nimesema hili, basi ushalijua. Kwani hakuna chochote kinachofichika kwako. Wewe unayajua yaliyomo ndani ya nafsi yangu, na mimi siyajui yaliyomo ndani ya nafsi yako. Hakika yako wewe Ndiye Mjuzi wa kila kitu, kilichojificha au kuwa wazi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net