Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 109

Al-Maaida 5:109

المائدة

يَوْمَ يَجْمَعُ ٱللَّهُ ٱلرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَآ أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا۟ لَا عِلْمَ لَنَآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّـٰمُ ٱلْغُيُوبِ

Maana

Siku ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya Mitume na awaambie: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatujui; hakika Wewe ndiwe Mwenye kujua yote yaliyofichikana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ile siku ambayo Mwenyezi Mungu atapo wakusanya Mitume awaambie: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatuna ujuzi; hakika Wewe ndiye Mjuzi Mkubwa wa yote yaliyo fichikana. [109]

[109] Nanyi ikumbukeni Siku ya Kiyama pale Mwenyezi Mungu atapo wakusanya mbele yake Mitume wote akawauliza: Hao kaumu zenu niliyo kutumeni kwao wamekujibuni nini? Waliamini au walikanya? Na hao kaumu wakati huo watakuwa wamehudhuria ili hoja iwe juu yao kwa ushahidi wa Mitume wao wakisema: Hakika sisi hatujui yaliyo tokea baada yetu kwa hao ulio tupeleka kwao. Ni Wewe peke yako ndiye unaye jua hayo, kwa kuwa Wewe ndiye uliye kusanya ujuzi wa vilivyo fichikana kama unavyo jua viliyo dhaahiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ikumbukeni, enyi watu, Siku ya Kiyama, siku Allah Mtukufu atakapo kuwakusanya Mitume, amani iwashukie, na awaulize kuhusu majibu ya watu wao waliyoyapata, pindi walipowalingania kwenye tawḥîd (kumpwekesha Allah Mtukufu). Na wao watajibu, «Hatuna ujuzi, sababu hatuyajui yaliyomo ndani ya nyoyo za watu wala yale waliyoyazua baada yetu. Hakika yako wewe ni Mjuzi wa kila kitu kilichofichika na kilicho wazi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net