Al-Maaida 5:108
المائدةذَٰلِكَ أَدْنَىٰٓ أَن يَأْتُوا۟ بِٱلشَّهَـٰدَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَآ أَوْ يَخَافُوٓا۟ أَن تُرَدَّ أَيْمَـٰنٌۢ بَعْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱسْمَعُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ
Hivyo ni karibu zaidi na kwamba watatoa ushahidi ulio sawa au wataogopa visije vikaletwa viapo vingine baada ya viapo vyao. Na mcheni Mwenyezi Mungu na msikie. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu ya wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hivi inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi ulio sawa au wataogopa visije vikaletwa viapo vingine baada ya viapo vyao. Na mcheni Mwenyezi Mungu na msikie. Na hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi wapotofu. [108]
[108] Hukumu hii ndiyo njia ya karibu mno ya kuwezesha mashahidi watoe ushahidi ulio sawa kwa kuhifadhi kiapo chao kwa Mwenyezi Mungu, au kwa kuogopa kufedheheka kwa kudhihiri uwongo wao, pindi ikiwa warithi watakula yamini kupinga kiapo chao. Nanyi mumuangalie sana Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu na amana zenu, na zit'iini hukumu zake, na muwe radhi nazo. Kwani katika hayo ndiyo yanapatikana maslaha yenu. Na msikhalifu hukumu za Mwenyezi Mungu, msije kutoka kwenye ut'iifu wake, kwani Yeye hamnafiishi kwa uwongzi wake mwenye kutoka katika ut'iifu wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hukumu hiyo ya kuapa baada ya Swala na kutokubali ushahidi wa hao wawili, baada ya kuutilia shaka, ndiyo inayouleta karibu zaidi uwezekano wa wao kutoa ushahidi kama ulivyo kwa kuogopa adhabu ya Akhera au kwa kuchelea yamini lao la urongo lisikataliwe na wale wenye haki baada ya kuapa kwao na asije akafedheheka yule mrongo ambaye yamini lake lilikakataliwa hapa ulimwenguni baada ya kufunuka uhaini wake. Na muogopeni Allah Mtukufu, enyi watu, na mumtunze msije mukaapa kiapo cha urongo na msije mkanyakuwa kwa mayamini yenu mali ya haramu. Na msikie mnayowaidhiwa nayo. Na Allah Mtukufu Hawaongozi watu wenye nyendo mbaya waliotoka nje ya utiifu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net