Al-Maaida 5:107
المائدةفَإِنْ عُثِرَ عَلَىٰٓ أَنَّهُمَا ٱسْتَحَقَّآ إِثْمًا فَـَٔاخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ ٱلَّذِينَ ٱسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلْأَوْلَيَـٰنِ فَيُقْسِمَانِ بِٱللَّهِ لَشَهَـٰدَتُنَآ أَحَقُّ مِن شَهَـٰدَتِهِمَا وَمَا ٱعْتَدَيْنَآ إِنَّآ إِذًا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Lakini ikigundulika kuwa wawili hao wamestahiki dhambi, basi wawili wengineo kutokana na warithi wenye kudai haki washike mahali pa wale wa mwanzo. Nao waape kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hakika ushahidi wetu ni wa haki zaidi kuliko ushahidi wa wale. Na sisi hatujafanya dhambi; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ikigundulikana kuwa wawili hao wamestahiki dhambi, basi wawili wengineo kutokana na warithi wenye kudai haki washike makamo ya wa mwanzo. Nao waape kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hakika ushahidi wetu ni wa haki zaidi kuliko ushahidi wa wale. Na sisi hatujafanya dhambi; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa walio dhulumu. [107]
[107] Na ikionekana kuwa mashahidi wawili hao wamesema uwongo katika ushahidi wao, au wameficha kitu, basi walio na haki zaidi kushika mahala pao ni wawili wengine walio karibu zaidi kukhusika na warithi wa maiti. Hao washike pahala pao baada ya Swala, wadhihirishe uwongo wa walio tangulia, na waape kwa Mwenyezi Mungu kuwa wale mashahidi wa mwanzo walisema uwongo, na: Yamini yetu inafaa zaidi kuliko yamini ya wale, na wala hatuitupi haki katika yamini zetu, wala hatuwatuhumu mashahidi wale kwa uzushi. Kwani tukifanya hivyo tutakuwa katika walio dhulumu, wenye kustahiki adhabu ya mwenye kumdhulumu mwenginewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakigundua wanaohusika na maiti kuwa wale mashahidi wawili wamefanya makosa ya hiana katika ushahidi au wasia, basi na wasimame mahali pao pa ushahidi watu wawili wenye ujamaa na aliyekufa waape kwa Allah Mtukufu: Ushahidi wetu wa kweli unastahiki zaidi kukubaliwa kuliko ushahidi wao wa urongo. Na sisi hatukukiuka haki katika kutoa ushahidi wetu. Na tukifanya dhuluma na kutoa ushahidi usio wa haki, basi sisi tutakuwa ni miongoni mwa madhalimu wenye kukiuka mipaka ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net