Al-Maaida 5:106
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ شَهَـٰدَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ حِينَ ٱلْوَصِيَّةِ ٱثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ ءَاخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِى ٱلْأَرْضِ فَأَصَـٰبَتْكُم مُّصِيبَةُ ٱلْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِنۢ بَعْدِ ٱلصَّلَوٰةِ فَيُقْسِمَانِ بِٱللَّهِ إِنِ ٱرْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِى بِهِۦ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَـٰدَةَ ٱللَّهِ إِنَّآ إِذًا لَّمِنَ ٱلْـَٔاثِمِينَ
Enyi mlioamini! Yanapomfikia mauti mmoja wenu na akataka kutoa wasia, basi wawepo mashahidi wawili miongoni mwenu ambao ni waadilifu. Na mnapokuwa katika safari, na msiba wa mauti ukawasibu, basi washuhudie wengineo wawili wasiokuwa katika nyinyi. Mtawazuia wawili hao baada ya Swala na waape kwa Mwenyezi Mungu, mkitilia shaka, wakisema: Hatutopokea thamani yoyote kwa haya hata kwa ajili ya jamaa; na wala hatutaficha ushahidi wa Mwenyezi Mungu; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Yanapo mfikia mauti mmoja wenu na akataka kutoa wasia, basi wawepo mashahidi wawili miongoni mwenu ambao ni waadilifu. Na mnapo kuwa safarini, na msiba wa mauti ukakusibuni, basi washuhudie wengineo wawili wasio kuwa katika nyinyi. Mtawazuia wawili hao baada ya Sala na waape kwa Mwenyezi Mungu, mkitilia shaka, wakisema: Hatutopokea thamani yoyote kwa haya hata kwa ajili ya jamaa; na wala hatutaficha ushahidi wa Mwenyezi Mungu; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi. [106]
[106] Enyi mlio amini! Mmoja wenu anapoona alama za kukaribia mauti na akataka kuusia lolote basi kushuhudia wasia huo iwe: kushuhudia watu wawili waadilifu katika jamaa zenu, au watu wawili wengineo ikiwa mmo safarini na ishara za mauti zikatokea. Wazuieni wawili hao baada ya Swala wanapo kusanyika watu, na waape kwa jina la Mwenyezi Mungu wakisema: Hatubadilishi kwa kiapo chake kwa chochote, hata ikiwa ni kutufaa sisi au yeyote katika jamaa zetu. Wala hatutaficha ushahidi alio tuamrisha Mwenyezi Mungu kuutimiza baraabara. Kwani tukificha ushahidi au tukasema lisio la kweli, tutakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu na kustahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi ambao mmemuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, mmoja wenu akiwa karibu na kufa, basi ni juu yake awashuhudishe wasia wake waaminifu wawili miongoni mwa Waislamu, au wawili wengine miongoni mwa wasiokuwa Waislamu ikibidi hivyo kama hakuna waislam Hao mtawashuhudisha iwapo muko safarini kwenye ardhi na mkafikiwa na kifo. Na iwapo mtautilia shaka ushahidi wao, wasimamisheni baada ya Swala, yaani, swala ya Waislamu, hasa Swala ya Alasiri, waape kwa Allah Mtukufu kiapo cha dhati kwamba wao hawachukui kwa ushahidi wao thamani ya kilimwengu kama badala, wala hawamfanyii mapendeleo jamaa yao na wala hawafichi kwa kiapo chao ushahidi wa Allah Mtukufu uliyoko kwao na kwamba wao wakilifanya hilo, basi wao watakuwa ni miongoni mwa waliofanya hatia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net