Al-Maaida 5:105
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا ٱهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Enyi mlioamini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hatawadhuru mwenye kupotoka ikiwa nyinyi mmeongoka. Ni kwa Mwenyezi Mungu ndiyo marejeo yenu nyote; kisha atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni walio potoka ikiwa nyinyi mmeongoka. Ni kwa Mwenyezi Mungu ndio marudio yenu nyote; basi atakwambieni yale mliyo kuwa mkiyatenda. [105]
[105] Enyi mlio amini! Fanyeni pupa ya kwendea kwenye matengenezo ya nafsi zenu kwa kumt'ii Mwenyezi Mungu. Upotovu wa mwengineo hautakudhuruni ikiwa nyinyi mmo kwenye uwongofu na mnalingania Haki. Na nyote nyinyi marejeo yenu ni Mwenyezi Mungu peke yake Siku ya Kiyama. Hapo atakupeni khabari ya vitendo vyenu, na kila mmoja wenu atamlipa kwa aliyo yatanguliza, na wala hapana hata mmoja atae shikwa kwa dhambi za mwenginewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi ambao mmemuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, jilazimisheni nafsi zenu kujishughulisha kumtii Allah Mtukufu na kujiepusha na kumuasi na endeleeni daima kufanya hivyo, hata kama watu hawatakubaliana na nyinyi. Mkifanya hivyo, hautawadhuru nyinyi upotevu wa mwenye kupotea madhali nyinyi mnajilazimisha na njia ya usawa, mnaamrisha mema na mnakataza maovu. Kwa Allah Mtukufu ndiko marejeo yenu nyote kesho Akhera, huko atawapa habari ya matendo yenu na atawapa malipo yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net