Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 104

Al-Maaida 5:104

المائدة

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ قَالُوا۟ حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ ءَابَآءَنَآ ۚ أَوَلَوْ كَانَ ءَابَآؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْـًٔا وَلَا يَهْتَدُونَ

Maana

Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na kwa Mtume, wanasema: Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo ambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, na kwa Mtume, husema: Yanatutosha tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?. [104]

[104] Na hawa makafiri wakiambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Qur'ani, na aliyo yaeleza Mtume, ili mpate kuongoka kwa kuyafuata, wao husema: Yanatutosha tuliyo wakuta nayo baba zetu. Yawafalia hawa kusema hayo? Ijapo kuwa hao baba zao ni kama nyama hoa, hawajui lolote la haki, wala hawaijui njia ya kuendea yaliyo sahihi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa makafiri, wanaoharamisha yaliyohalalishwa na Allah Mtukufu, wanapoambiwa, Njooni kwenye hukumu zilizoteremshwa na Allah Mtukufu na uamuzi wa Mtume Wake, ili halali na haramu ziwafunukie, wao huwa wakisema, «Yanatutosha yale tuliyoyarithi kwa baba zetu ya maneno na vitendo.» Je wanayasema hayo ingawa baba zao walikuwa hawajui chochote: yaani, hawaielewi haki, hawaitambui wala hawaongoki kuifikia? Basi vipi watawafuata na hali ni hii? Kwa kweli, hakuna mwenye kuwafuata isipokua mjinga zaidi kuliko wao na mpotevu zaidi wa njia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net