Al-Maaida 5:1
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَوْفُوا۟ بِٱلْعُقُودِ ۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ ٱلْأَنْعَـٰمِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّى ٱلصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ
Enyi mlioamini! Timizeni mapatano. Mmehalalishiwa wanyama wa kufugwa, isipokuwa wale mnaosomewa. Lakini msihalalishe kuwinda hali ya kuwa mko katika Ihram. Hakika, Mwenyezi Mungu anahukumu apendavyo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Timizeni ahadi. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo, ila wale mnao tajiwa. Lakini msihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Hija. Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu apendavyo. [1]
[1] Enyi Waumini! Jilazimisheni kutimiza ahadi zote baina yenu na Mwenyezi Mungu, na ahadi za kisharia zilio baina yenu na watu wengineo. Na Mwenyezi Mungu amekuhalalishieni kula nyama howa, yaani nyama wa kufuga, kama ngamia, ng'ombe, kondoo, mbuzi n.k. ila wale mlio tajiwa kuwa ni haramu. Wala haikujuzieni kuwinda barani pale mnapo kuwa mmeharimia Hija, au mpo katika eneo la ardhi takatifu. Hakika Mwenyezi Mungu huhukumu apendavyo kwa hikima yake. Yeye ndiye Muumbaji, na ndiye Mwenye kujua jema na baya la viumbe vyake. Na haya ni miongoni mwa ahadi za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, timizeni ahadi za Allah Mtukufu zilizotiliwa mkazo za kuamini Sheria za Dini na kuzifuata, na tekelezeni ahadi mlizopeana nyinyi kwa nyinyi miongoni mwa amana mlizowekeana, biashara na mengineyo kati ya yale yasiyoenda kinyume na Kitabu cha Allah Mtukufu na mafundisho ya Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie. Na hakika Allah Mtukufu Amewahalalishia wanyama wa mifugo, nao ni ngamia, ng’ombe na mbuzi na kondoo, isipokuwa yale ambayo Allah Mtukufu amewaelezea ya kuwaharamishia mfu, damu na mengineyo; na ya kuwaharamishia kuwinda mkiwa kwenye hali ya ihramu (kwa ibada ya Hija au Umra). Kwa hakika Allah Mtukufu Anahukumu Anachokitaka kulingana na hekima Yake na uadilifu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net