Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 9

Al-Hujuraat 49:9

الحجرات

وَإِن طَآئِفَتَانِ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٱقْتَتَلُوا۟ فَأَصْلِحُوا۟ بَيْنَهُمَا ۖ فَإِنۢ بَغَتْ إِحْدَىٰهُمَا عَلَى ٱلْأُخْرَىٰ فَقَـٰتِلُوا۟ ٱلَّتِى تَبْغِى حَتَّىٰ تَفِىٓءَ إِلَىٰٓ أَمْرِ ٱللَّهِ ۚ فَإِن فَآءَتْ فَأَصْلِحُوا۟ بَيْنَهُمَا بِٱلْعَدْلِ وَأَقْسِطُوٓا۟ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُقْسِطِينَ

Maana

Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi, basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki. [9]

[9] Na ikiwa makundi mawili ya Waumini yanapigana, basi enyi Waumini, yapatanisheni. Ikiwa moja ndilo linalishambulia la pili, na likakataa kupatanishwa, basi lipigeni hilo linalo shambulia, mpaka lirejee kwenye hukumu ya Mwenyezi Mungu. Likirejea basi wapatanisheni kwa insafu. Na fanyeni uadilifu baina ya watu wote katika kila jambo. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wenye kufanya uadilifu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makundi mawili ya Waumini yakipigana, fanyeni upatanishi, baina yao kwa kuyaita yakubali kuamuliwa na Kitabu cha Allah Mtukufu na (Sunnah) za Mtume Wake, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na kuridhika na uamuzi wa hivyo viwili. Iwapo kundi mojawapo ya yale mawili litalifanyia uadui kundi lingine na litakataa kukubali mwito huo wa upatanishi, basi lipigeni vita mpaka lirudi kwenye uamuzi wa Allah Mtukufu na Mtume Wake, na likirudi fanyeni upatanishi baina ya hayo mawili kwa haki, na mfanyeni uadilifu katika uamuzi wenu kwa kutotoka nje ya hukumu ya wenyezi Mungu na hukumu ya Mtume Wake katika uamuzi wenu. Hakika Allah Mtukufu Anawapenda waadilifu katika uamuzi wao, wanaohukumu baina ya viumbe Vyake kwa haki. (Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya mapenzi kwa Allah Mtukufu kihakika, kama inavyonasibiana na utukufu Wake Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net